MDAHALO WA VIJANA NI NINI
?
Ni uwanja pekee unaotupa fursa Vijana na Watoto wa Tanzania
kukaa pamoja ili kujadili mambo muhimu ya kijamii yanayo tugusa .Hii
ni pamoja na kujaribu kutafuta suluhisho la Baadhi ya matatizo
yanayoikumba Jamii ,Hususani Vijana na Watoto.
Baadhi ya matatizo ya Kiuchumi na Kijamii yanayo jadiliwa ni
pamoja na ,Suala zima la Umasikini ,Mazingira Magongwa hususani
Gongwa hatari la Ukimwi,Siasa ,Haki za Binaadamu,Elimu na Masuala
yote yanayo mtatiza Mwananchi.
HISTORIA FUPI.
Mdahalo huu ulianza mnamo miaka miwili iliyopita ,Chanzo kikiwa
ni Mawazo ya Wanafunzi wa Mkoa wa Dar es salaam ,Kukaa pamoja ili
kutafuta mbinu za kuchangia katika maendeleo ya jamii yetu kwa
njia moja au Nyingine .
Baada ya muda mfupi tuliokuwa Wanafunzi tuligundua kuwa
tutakuwa hatujawatendea haki Vijana walioko nje ya shule ,Hivyo
Tuliamua kutafuta sehemu ambayo itaweza kutunufaisha vijana wote
bila kujali tunakotoka ili mradi kwa Dhumuni moja la Ujenzi wa
Taifa .
Wazo letu lilipokelewa kwa mikono miwili na shilika la
Kimataifa la Kuudumia Watoto (UNICEF).Hawa walitupa nafasi ya
kuutumia Ukumbi wao wa mikutano kila Jumamosi ya Kwanza ya
Mwezi.Baada ya kuzigundua Juhudi zetu,Sasa UNICEF wanatusaidia
katika masuala mbalimbali,mfano,Gharama zote za Uendeshaji.
DHUMUNI.
Dhumuni kuu ni kuwaweka Vijana na watoto pamoja ili waweze
kufanya maamuzi ya maendeleo ya Jamii yao kwa sauti moja.Kwa
kuzingatia Takwimu zilizopo,tuliono Vijana na Watoto ndio wengi
katika Jumla ya watu Hapa Tanzania,Hivyo maamuzi ya busara kutoka
kwa Vijana na Watoto ni mchango mkubwa wa maendeleo ya Taifa letu.
Vijana tunaizingatia Methali ya Kichina isemayo kuwa ,``Kama
watu elfu moja watapiga risasi wakilenga shabaha moja tu na kwa
wakati mmoja,huna sehemu ya shabaha ambayo haitapigwa’’.
Hivyo wachache tuliona ni Busara tuwahamasishe Vijana wenzetu
ili tuwe wengi,kusudi tunapolenga shabaha kwa wakati mmoja ,isibaki
sehemu isiyopigwa.
Pia tumezingatia wito wa Rais wetu,Mheshimiwa Benjamin Mkapa ,unaotaka
mipango yote ya maendeleo itokane na wananchi wenyewe badala ya
kutoka Serikali Kuu.Hivyo tunaiona ni fursa muhimu kwetu kama
Vijana kuweza kutoa mchango wetu katika maendeleo (Shukrani nyingi
kwa Mheshimiwa Rais)
Pamoja na hilo Mdahalo wa Vijana una dhumuni kubwa la
kuhamasisha maendeleo ya Vijana kupitia njia mbalimbali kama
ifuatavyo;-
(a)Kuiunganisha Serikali na mashilika yasiyo ya
Kiserikali(Non-Gorvernment Organizations),Mashilika ya kimataifa ,Vyombo
vya habari na Jamii kwa Ujumla ili kuongeza uelewa juu ya mambo
yanayo wahusu Vijana ,Mathalani dawa za kulevya, magonjwa,Ajira na
mengine mengi.
(b)Kuanzisha malengo endelevu yanayodhamilia kuwaendeleza na
kuwashilikisha Vijana wa jinsia zote
katika maendeleo ya taifa.
(c )Kuufanya Mdahalo wa vijana uwe nafasi ya Vijana kujifunza
mambo mbalimbali ya Jamii,mfano Haki za uchaguzi,Wajibu na haki za
Binadamu na mengine kama hayo .
(d)Kuwashauri Vijana,waweze kutumia maliasili tulizonazo nchini
ili kutatua matatizo yetu ya Kijamii na kiuchumi.
(e)Kuishauri Serikali katika masuala yote yanayowahusu
Vijana,hususani Haki na Wajibu wa Vijana katika jamii.
(f)Kuwaunganisha Vijana wote wa Tanzania kwa malengo ya
kuvumbua na kuendeleza Vipaji vyao.
MIKAKATI ILIYOPO.
(1)Kuakikisha malengo /madhumuni ya mdahalo huu wa Vijana
yanafikiwa na Vijana wenyewe kwa faida yao na jamii kwa ujumla.
(2)Tuna mpango wa kuanzisha ushirikiano wa Vijana wa Nchi za
Afrika Mashariki na baadae Afrika ya Kati ili Kubadilishana uzoefu
katika utatuzi wa matatizo yanayo wakabili Vijana,hususani suala
zima la ugonjwa wa Ukimwi ,Vita na Madawa ya kulevya.
(3)Tunao mpango wa kuishawishi Serikali pamoja na mashilika ya
kimataifa kutusaidia kuitisha mkutano wa Vijana wa Afrika
mashariki na Kati ili tutumie nafasi hiyo Kuongelea suala la
Vita.Lengo kuu likiwa ni kuwashawishi na kuwashauri Vijana Wenzetu
wa nchi zenye Vita kama vile,Rwanda ,Burundi,Jamuhuri ya watu wa
Congo na Uganda,wasikubali kushilikishwa katika vita ili njia hiyo
isaidie kupunguza vita katika Nchi zao.
Mkakati huo bado tuna ujadili kwani ni mkakati wa
gharama.Lakini tuna mpango wa kuwaomba UNICEF na Mashilika mengine
ya kimataifa yanayo hudumia nchi zenye Vita,Kutusaidia kwa hali na
mali kufikia lengo letu .
(4)Tunao mgo wa kuiomba serikali nafasi ya kuwa tunashiriki
katika mikutano mikuu, hasa linapokuja suala la kuwakeana mikataba
ya Amani kwa Nchi zenye matatizo ya Vita,ili nasi tuweze kutoa
ushawishi na kilio chetu kwa hao wanao ng’ang’ania vita,ili
waone ni kwa kiasi gani Vita inawaumiza na Kuwaathili kwa kiasi
kikubwa Vijana wenzetu katika nchi hizo.
MAFANIKIO.
/1/ Kama Vijana, tumeweza kushiriki katika maamuzi mbalimbali
ya Taifa, Kwa mfano,Tulishiriki vema katika urekebishaji wa Sera
ya vijana ,tunaishukuru Wizara ya kazi , Michezo na maendeleo ya
Vijana kwa kutushirikisha katika maamuzi hayo.
/2/ Vijana wenzetu wachache walifanikiwa kupeleka ripoti juu ya
Umasikini katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee
wakati wa wiki ya sera ya umasikini (Poverty Policy Week).
/3/ Tumefanikiwa kuwaunganisha Vijana kwa asilimia zipatazo 55%
,Kwani kupitia katika Tovuti (Website)
www.youthdialogue.gobot.com ,tuliyo ianzisha, Vijana kutoka
sehemu mbalimbali za Tanzania wameweza kujua lengo letu na sasa
wanatoa maoni yao .Tovuti hiyo ni changa moto kwa vijana wote
nasasa tuko katika mkakati wa kuitangaza ili na wenzetu kutoka Nje
ya Tanzania waweze kuungana nasi.
/4/ Ushirikiano kati ya Vijana na Watoto umekuwa madhubuti
kwani wamefikia kuwa na uwezo wa kuendesha vipindi vyao katika
Radio na T.V, hali ambayo imewapatia fursa ya kuzijua haki zao
nawajibu wao miongoni mwa jamii.
/5/ Tumekuwa mstari wa mbele kutoa ujumbe na kujadili mambo
mbalimbali katika siku maalumu kupitia vyombo vya Habari
mfono,Siku ya Mtoto wa Africa,siku ya Ukimwi duniani,Wiki ya
umasikini na nyinginezo .
/6/ Kikubwa tumefanikiwa kufanya mdahalo huu uwe uwanja wa
mafunzo kwa Vijana wenzetu,kwani kwa kipindi hiki kifupi wote tume
elimishwa mambo mbalimbali kama ifuatavyo ,
(a).Rushwa [Afisa kutoka kitengo cha kuzuia Rushwa ]
(b).Utandawazi na mawasiliano
(c). Uwakilishi wa kijana bungeni [Mheshimiwa Lazaro Nyalandu
MP]
(d).Tanzania bila umasikini .
(e)Uboreshwaji wa Sera ya Vijana ya mwaka 1996
Mwisho tunatoa shukrani za dhati kwa wote wanaoshirikiana nasi
katika kulisukuma Gurudumu la Maendeleo.Shukrani za pekee
ziwaendee serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kutushilikisha kama njia moja wapo ya kutuwezesha.UNICEF ni ndugu
zetu wa damu ambao vijana wote kwa Sauti moja,tunamuomba Mungu
awasaidie ili nasi tuweze kufikia Malengo yetu.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
Waandaji;-
FRANK RICHARD
ARNOLD KAYANDA
ATHANAS WILLIAM